Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
2013-01-17
Date of
Establishment:
huo Kikuu cha Dar es Salaam - Taasisi ya Confucius kilianzishwa kwa ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Walimu cha Zhejiang (Zhejiang NormaL University), China na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania, mnamo Januari 2013. Kufikia mwaka 2025, taasisi hiyo imeanzisha vituo vya kufundishia 14 nchini Tanzania.
Taasisi ya Confucius inatoa kozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na:
Kozi ya shahada ya ualimu kwa lugha ya Kichina na Kiingereza,
Kozi ya diploma ya Kichina,
Kozi ya Kichina ya hiari,
Mafunzo ya Kichina Kwa vitendo,
Kozi ya sanaa ya mapigano (Wushu),
Kozi za maandalizi ya mtihani wa HSK,
Kozi ya nyimbo za Kichina,
Na kozi za dansi.
Kufikia mwaka 2025, idadi ya wanafunzi walioshiriki katika mafunzo ya taasisi hiyo inakadiriwa kufikia karibu watu 50,000, na imeandaa zaidi ya matukio ya kitamaduni 500, yaliyoifikia hadhira ya zaidi ya watu 110,000.
Mwaka 2017, Taasisi ya Confucius ya Dar es Salaam ilitunukiwa tuzo ya "Taasisi ya Confucius Bora". Aidha, katika miaka ya 2017, 2018, 2019, 2021, 2023, na 2024, taasisi hiyo ilitambuliwa kama “Kituo bora cha mitihani ya lugha ya Kichina (HSK)”.
Mkurugenzi wa kwanza na wa tatu wa upande wa China, Zhang Xiaozhen, alitunukiwa tuzo ya “Mtu Binafsi Bora wa Taasisi ya Confucius” na tuzo ya “Mtu wa Mwaka katika Uenezi wa Utamaduni wa Kichina - Mwanga wa Uchina” mnamo mwaka 2013. Mwaka 2016, alichaguliwa kuwa mmoja wa watu 60 muhimu katika uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Afrika, na mwaka 2024 alichaguliwa kuwa mmoja wa watu 60 muhimu katika uhusiano kati ya China na Tanzania, pamoja na kutunukiwa Medali ya Ukumbusho kwa Wakurugenzi wa Taasisi ya Confucius.
Mkurugenzi wa pili kutoka China, Liu Yan, alipata tuzo ya "Nuru ya Ustaarabu. Mtu Bora wa Mwaka wa Ubadilishanaji wa Utamaduni wa China 2018".